Tetesi

Scalvini, Koopmeiners nyota yang’ara

Manchester United, Juventus na Real Madrid zote zinafuatilia uchezaji wa nyota wa Atalanta Giorgio Scalvini na Teun Koopmeiners.

Wachezaji hao wanafikiriwa kuwa mojawapo ya mabeki bora zaidi vijana Ligi Kuu Italia, Serie A.(Alfredo Pedulla)

Juventus na Newcastle United zinatarajiwa kuongoza mbio kumsajili Kalvin Phillips kutoka Man City.

Kiungo huyo anatarajiwa kuondoka Etihad Januari 2024 kwenda klabu nyingine kutafuta muda zaidi wa kucheza.(Football Insider)

Tottenham Hotspur ina nia kumsajili Diminic Solanke iwapo itashindwa dili kupata saini ya Evan Ferguson kutoka Brighton & Hove Albion.(The Sun)

Inter ipo katika mazungumzo na Club Brugge kumsajili Tajor Buchanan. Mchezaji huyo, 24, anaonekana kama mbadala wa Juan Cuadrado.(Fabrizio Romano)

Related Articles

Back to top button