Baada ya vigogo, Kyombo atafuta ufufuo Polisi

KILIMANJARO: MSHAMBULIAJI Habibu Kyombo ameanza safari mpya ya kujaribu kurejesha makali yake baada ya kuibukia Polisi Tanzania, kufuatia kupitia katika klabu mbalimbali kubwa ndani na nje ya nchi.
Kyombo amejiunga na Polisi Tanzania akitokea Mbeya City, akiwa na uzoefu wa kucheza katika timu zenye majina makubwa ikiwemo Simba SC, Pamba Jiji na Singida Black Stars.
Mbali na safari yake ndani ya Tanzania, mshambuliaji huyo pia aliwahi kuvuka mipaka baada ya kujiunga na Napsa Stars ya Zambia na mabingwa wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.
Hata hivyo, akiwa Sundowns hakupata nafasi ya kutosha kuonesha uwezo wake, jambo lililomfanya kuendelea kutafuta sehemu ambayo itampa nafasi ya kurejesha makali yake uwanjani.
Sasa Polisi Tanzania imekuwa kituo chake kipya, huku akiwa na dhamira ya kuonesha kuwa bado ana uwezo wa kuwa mshambuliaji mwenye mchango mkubwa baada ya uzoefu alioupata katika safari yake ya soka.
Kyombo anatarajiwa kuwa sehemu ya mipango ya Polisi Tanzania katika kujenga kikosi cha ushindani msimu wa 2026/27. Polisi wapenda msimu huu wakitokea championship.




