
MICHEZO sita ya raundi ya kwanza Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)-FA inafanyika leo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Songwe, Mwanza na Shinyanga.
Klabu ya Alliance itakuwa mgeni wa Stand United katika uwanja wa Mwadui, Shinyanga wakati Tandika United itakabiliana na Cosmopilitan katika uwanja wa Bandari, Dar es salaam.
Polisi Sengerema itavaana na Mbao katika uwanja wa Nyamagana, Mwanza wakati Kahama Mabasi itamenyana na Mapinduzi katika uwanja wa Taifa, Shinyanga.
Magogo itakuwa mgeni wa Afya katika uwanja wa Vwawa, Songwe wakati KFC itavaana na THB katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.