Nyumbani

Mbulu mguu sawa UMITASHUMTA

WACHEZAJI 89 na walimu 10 wa wilaya ya Mbulu wamechaguliwa kushiriki mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi UMITASHUMTA) mkoa wa Manyara yanayoanza Mei 26.

Ofisa Michezo wa Halmashauri ya mji wa Mbulu Benson Maneno amesema wachezaji na viongozi hao watashiriki michezo hiyo ili kuunda timu ya mkoa ya UMITASHUMTA.

“Tumejipanga vyema kama Mbulu kuweza kutoa vijana watakaokuwa na uwezo kwenda kuwakilisha mkoa katika michezo ya Umitashumta taifa itakayofanyika mkoani Tabora mapema mwezi Juni,”amesema Maneno.

Amesema halmashauri ya mji wa Mbulu ni mabingwa wa jumla kwa upande wa soka na riadha katika michezo hiyo kwa Mkoa huo wa Manyara.

Wanafunzi 370 kutoka kanda za Nambis, Endagikot na Daudi walichuana vikali katika viwanja vya CCM Mbulu hivyo kupatikana wachezaji 89.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button