Nyumbani

Taoussi, Tchakei watwaa tuzo za Oktoba

DAR ES SALAAM: KOCHA wa Azam FC Rachid Taoussi amechaguliwa kuwa kocha bora huku mshambuliaji wa Singida Black Stars  Marouf Tchakei ametwaa tuzoya ya mchezaji bora wa Oktoba wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2024/25.

Taoussi aliyeingia Fainali katika mchakato huo pamoja na Abdulhamid Moallin wa KMC FC na Denis Kitambi wa Singida Black Stars, aliiongoza Azam FC kushinda michezo mitatu iliyocheza na kupanda kwa nafasi moja kutoka tano hadi nne. Azam FC ilizifunga Namungo 1-0, Tanzania Prisons 2-0  na Ken Gold 4-1.

Kwa upande wa Tchakei alionesha kiwango kizuri mwezi Oktoba akiwashinda Lusajo Mwaikenda wa Azam FC na Pacome Zouzoua  wa Yanga alioingia nao katika fainali ya tuzo za mwezi huo zinazoandaliwa na kamati ya Tuzo za Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF).

Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake kupata ushindi katika michezo mitatu kati ya minne aliyocheza;alifunga mabao matatu na kuhusika kwenye bao moja kwa dakika 360 alizochezea timu hiyo mwezi Oktoba mwaka huu.

Singida Black Stars ilizifunga Mashujaa FC bao 1-0,  Namungo FC mabao 2-0,  Fountain Gate 2-0 na ilipoteza kwa Yanga bao 1-0.

Related Articles

Back to top button