CHAN

Miezi 6 inatosha kuja kiutofauti  CHAN

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,  Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, amesema kuongezwa kwa miezi sita ya maandalizi ya mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) inatoa nafasi kuendelea kuwa bora kwa miumbo mbinu.

Kauli hiyo amesema Jumatano ya Januari 15, kwenye hafla ya Kongamanano la wadau wa Michezo kuelekea CHAN na fainali za AFCON 2027.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Jumanne, Januari 14, 2025, limetangaza kuahirishwa kwa michuano ya CHAN ambayo ilitakiwa kufanyika Februari 1 hadi 28 lakini sasa kusogezwa mbele hadi Agosti mwaka huu, Tanzania, Kenya na Uganda.

Mwana FA amesema muda wa miezi sita ya maandalizi inatoa fursa ya kujihakikishia mashindano hayo yanakuwa na utofauti mkubwa na kuacha alama nzuri.

“Tanzania tulikuwa tumefika kwa asilimia 90 ya maboresho ya uwanja na kuwa tayari kwa michuano hayo, lakini baada ya kupokea taarifa ya kusongezwa mbele kwa mashindano hayo inatoa muda wa kujipanga vizuri na mashindani hayo kuwa na utofauti na tulivyopanga,” amesema.

Naye Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji waSerikali, Gerson Msigwa amesema kusogezwa mbele kwa michuano ya  (CHAN) 2024, inatoa muda wa kuendelea maboresho makubwa zaidi ya viwanja.

“Tanzania tulishafanya maandalizi ya kutosha kwenye kiwanja cha Meja Jenerali Isamuhyo, Gymkhana na uwanja wa Law School vilikuwa tayari kwa asilimia 90.

“ Kusongezwa mbele kwa mashindano hayo tunapata nafasi ya kufanya vizuri katika ujezi wa viwanja vya mazoezi na kuboresha zaidi katika maeneo ya kuchezea na kufanya wa kuvutia zaidi,” amesema.

Related Articles

Back to top button