CHAN

CHAN 2025: Tanzania kuanza na Sudan

Tanzania imepangwa kuanzia ugenini dhidi ya Sudan katika mchezo wa raundi ya kwanza wa kufuzu fainali za CHAN 2024 zitakazofanyika mwakani katika mataifa ya Tanzania, Kenya na Uganda.

Kwa mujibu wa droo iliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) leo, Tanzania ikifanikiwa kuitoa Sudan itakutana na mshindi kati ya Eritrea na Ethiopia.

Droo hiyo imepangwa kwa kuzingatia kanda sita za CAF, kila kanda ikitarajiwa kutoa wawakilishi kwenye fainali hizo.

Mechi za mtoano zitachezwa raundi mbili, raundi ya kwanza itapigwa Oktoba 27 hadi 29 na kurudiana Novemba 1 hadi 3 mwaka huu huku mechi za raundi ya pili zikipigwa Desemba 20 hadi 22 na kurudiana Desemba 27 hadi 29 mwaka huu.

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, ni Uganda pekee itakayoanzia raundi ya pili ikisubiri mshindi kati ya Burundi na Somalia.

UNAF
Morocco, Libya na Tunisia zimefuzu moja kwa moja..
WAFU A
Raundi 1;
Sierra Leone vs Liberia
Raundi 2;
Sierra Leone / Liberia VS Senegal
Mauritania vs Mali
Guinea vs Guinea Bissau.

WAFU B.
Raundi 1
Togo vs Benin
Raundi 2
Togo/Benin vs Niger
Ivory Coast vs Burkina Faso
Ghana vs Nigeria

UNIFFAC (Zote zinaanzia raundi ya pili).
Equtorial Guinea vs Congo
Afrika ya Kati vs Cameroon
Chad vs DR Congo

CECAFA
Raound 1
Burundi vs Somalia
Ethiopia vs Eritrea
Sudan vs Tanzania
South Sudan vs Kenya
Djibouti vs Rwanda

Raundi 2;
Burundi/Somalia vs Uganda
Ethiopia/Eritrea vs Sudan/Tanzania
South Sudan/Kenya vs Djibouti/Rwanda

COSAFA
Raundi 1
Zimbabwe vs Eswatin
Lesotho vs Namibia
Raundi 2
Zimbabwe/Eswatin vs Madagascar
Lesotho/Namibia vs Angola
Mozambique vs Zambia

Related Articles

Back to top button