CHAN

Motsepe kutua nchini, kukagua Uwanja wa Benjamin Mkapa

DAR ES SALAAM: RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Afrika (CAF), Patrice Motsepe anatarajiwa kufanya ziara ya mataifa matatu, Tanzania, Kenya na Uganda ambayo yatakuwa wenyeji wa Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN), 2025.

Motsepe atafanya ziara hiyo Alhamisi Desemba 19 atakuwa jijini Dar es Salaam, Tanzania, kukagua Uwanja wa Benjamin Mkapa, ataenda Nairobi Kenya na Ijumaa Desemba 20 atakuwa Kampala nchini Uganda.

Katika ziara hiyo, atakutana na Serikali, viongozi wa soka la nchini husika na kamati ya maandalizi za kutoka nchi hizo tatu.Ziara na mikutano hiyo itakuwa sehemu ya kutembelea viwanja yanayofanyiwa ukarabati kabla ya mashindano ya 2025.

Motsepe inakuwa ziara yake ya pili ya ukaguzi wa mataifa hayo matatu iliyofanywa na ujumbe wa CAF, Novemba mwaka huu kwa kutembelea viwanja mbalimbali, maeneo ya mazoezi, hotel, viwanja vya ndege na kufanya ukaguzi wa vifaa vingine

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button