Ligi Ya Wanawake

Ligi ya wanawake kinawaka leo

Pazia la Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) kwa msimu wa 2024/2025 linafunguliwa leo kwa viwanja vitano kuwa shughulini mechi zote zikipigwa majira ya saa 10 jioni.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba Queens watakuwa katika uwanja wa kituo cha ufundi cha shirikisho la soka nchini TFF Kigamboni Dar es Salaam, wakiikaribisha Mlandizi Queens huku watani wao Yanga princess wakiwa ugenini katika dimba la Karume mkoani mara dhidi ya Bunda Queens

Mabingwa wa ngao ya jamii ya ligi hiyo JKT Queens wao watakuwa katika dimba CCM Kirumba jijini Mwanza ambako watakuwa wageni wa Alliance Girls. Wanajeshi wenzao Mashujaa Queens watalitawala dimba la Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni jijini Dar es Salaam dhidi ya Gets Program.

Wakuza vipaji Fountain Gate Princess waliodhamiria kufanya mapinduzi ya soka la wanawake msimu huu wataanza kampeni hiyo dhidi ya Ceaciaa Queens uwanja wa Jamhuri Dodoma

Related Articles

Back to top button