Ligi Ya WanawakeNyumbani
JKT Queens kuendeleza ubabe SLWPL?

LIGI Kuu ya soka Wanawake Tanzania Bara (SLWPL) inaendelea leo kwa mchezo mmoja Dar es Salaam.
Katika mchezo huo JKT Queens itakuwa mwenyeji wa Mkwawa Queens kwenye uwanja wa Maj Gen Isamuhyo.
JKT Queens ipo nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 18 baada ya michezo 8 wakati Mkwawa Queens ipo nafasi ya 10 mwisho wa msimamo ikiwa na pointi 1.
Februari 15 kumefanyika michezo mitatu ya SLWPL ambapo Yanga Princess imeichapa Amani Queens mabao 3-0 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Fountain Gate Princess imeiangushia kipigo kikali The Tigers Queens cha mabao 6-0 huku Alliance Girls na Baobab Queens zikienda suluhu.