Ligi Ya Wanawake

Simba Queens kulipambania Taifa Ethiopia

DAR ES SALAAM: KIKOSI Cha Simba Queens kimesafiri leo kuelekea nchini Ethiopia kwa matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya kutafuta mwakilishi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake.

Simba Queens inayonolewa na Kocha Juma Mgunda akisaidiana na Mussa Hassan ‘Mgosi’ wakiwa na imani kubwa ya kikosi cha timu hiyo kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Kocha mkuu Mgunda amesema kuwa wamefanya maandalizi mazuri kuelekea michuano ya CECAFA na timu yake ipo tayari kwa ajili ya kuiwakilisha vema Tanzania na klabu ya Simba.

Amesema wana kikosi imara na usajili wa nyota wapya waliosajiliwa dirisha kubwa wanaongeza kitu ndani ya timu hiyo na anaimani kubwa ya kufanya vizuri katika michuano hiyo kwa ajili ya kukata tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Wachezaji wana morali ya kwenda kufanya vizuri ili kutwaa ubingwa huo utatupa tiketi ya kuiwakilisha CECAFA kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Mgunda.

Amesisitiza kikosi cha Simba kitafika Ethiopia siku mbili kabla ya kuanza michuano ili kuwapa wachezaji muda wa kuzoea mazingira na hali ya hewa ya nchini hiyo.

Simba Queens itaanza kujitetea Agosti 18, 20 na 22, 2024, kwa kucheza Afad Djibouti kutoka Djibouti, mchezo wa pili dhidi ya Kawempe Muslim. ,mchezo wa mwisho RVP Buyenzi, michezo yote kucheza uwanja wa Abebe Bikila, nchini humo.

Related Articles

Back to top button