Ligi Ya Wanawake

Agnesi Pallangyo awatuliza mashabiki

DAR ES SALAAM: MCHEZAJI wa Yanga Princess Agnesi Pallangyo amewatuliza mashabiki kutokuwa na hofu dhidi ya mwenendo wao kwenye Ligi Kuu ya Wanawake akisema licha ya timu kufanya vibaya katika baadhi ya michezo hawawezi kushuka daraja.

Yanga princess imetoka kupoteza mchezo uliopita hivi karibuni dhidi ya JKT Queens mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa KMC Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili Agnesi alisema kupoteza mchezo kunawaumiza kwasababu siku zote hujiandaa kwa ajili ya kushinda.

“Malengo yetu siku zote ni kushinda mchezo wowote mbele yetu, unapopoteza lazima uumie , lakini haimaanishi tutashuka daraja, Bado tuna safari ndefu tutajipanga kwa michezo iliyoko mbele yetu,”alisema.

Nyota huyo alisema: “Mashabiki wasikate tamaa, tunajua wanaumia na hata sisi tunaumia pia, malengo yetu ni kufanya vizuri, tutajitahidi katika michezo ijayo naamini tutafanya vizuri,”

Kwa mujibu wa Agnesi, baada ya mchezo huo baadhi ya wachezaji walilia kwa uchungu kuonesha kwamba hawakubaliani na matokeo lakini ndio matokeo yalitowakuta.

Related Articles

Back to top button