Bundesliga

Kompany: Tupo njia sahihi

MUNICH: Kocha mkuu wa ‘Wabavaria’ Bayern Munich Vincent Kompany amesema anaamini kikosi chake kipo katika mwelekeo sahihi licha ya kutoonja ladha ya ushindi katika takriban mechi 3 za hivi karibuni.

Kikosi cha Bayern hakijawa na mwenendo mzuri katika siku za hivi karibuni baada ya kula kichapo dhidi ya Aston Villa kwenye Ligi ya mabingwa barani Ulaya na sare mbili dhidi ya Bayer Leverkusen na Eintracht Frankfurt kwenye Bundesliga.

“Tunajua tunapaswa kufanya vizuri zaidi lakini tuna imani asilimia 100 kwamba lengo letu litafanikiwa, tupo kwenye njia sahihi. Tunatumai, tutapiga hatua kwenda mbele katika mchezo ujao,” alisema Kompany katika mkutano na waandishi wa habari.

“Natoka Ubelgiji hivyo sisi pia tunapenda kujifunza kama Wajerumani tu ninayosema sio imani tu ni tathimini tulitawala mchezo wetu dhidi ya Aston Villa na Frankfurt tulikuwa na nafasi nyingi zaidi yao tumejifunza kutokana na hilo na tutapambana kuhakikisha tunashinda” aliongeza

Bayern Munich watakuwa Allianz Arena Jumamosi hii dhidi ya VfB Stuttgart kabla ya kuanza wiki ya ligi ya mabingwa dhidi ya Barcelona ugenini Nou Camp siku ya Jumatano wiki ijayo

Related Articles

Back to top button