Bundesliga

Sule atangaza kustaafu soka

BERLIN: BEKI wa Borussia Dortmund, Niklas Sule ametangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu huu baada ya kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara.

Sule mwenye umri wa miaka 30 amesema amefikia uamuzi huo baada ya kuumia goti katika mchezo dhidi ya TSG Hoffenheim mwezi uliopita.

Beki huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani- aliyewahi kucheza mechi 49 za kimataifa, amesema alitafakari sana kuhusu mustakabali wake kabla ya kuamua kutundika daruga.

“Nilipofanyiwa kipimo cha MRI siku iliyofuata na kuambiwa kuwa haikuwa majeraha ya goti, nilijua moja kwa moja kuwa muda wangu umefika,” amesema Sule.

Amesema hakuwa tayari kuendelea kuishi kwa hofu ya kupata tena majeraha makubwa ya goti ambayo yangemzuia kufurahia maisha yake binafsi na familia.

Sule alianza maisha yake ya soka akiwa Hoffenheim kabla ya kujiunga na Bayern Munich mwaka 2017 ambako alishinda mataji matano ya Bundesliga pamoja na UEFA Champions League mwaka 2020.

Mwaka 2022 alihamia Dortmund ambako ameendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho hadi alipotangaza uamuzi wake wa kustaafu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button