Ligi KuuNyumbani

Mwambusi awatuliza mabosi Ihefu

KOCHA mpya wa Ihefu, Juma Mwambusi amewataka viongozi wa timu hiyo kuondoa hofu akisema pamoja na kuanza vibaya msimu nafasi ya kurekebisha makosa ipo.

Akizungumza na Spotileo, kocha huyo ambaye amechukua nafasi ya Zuber Katwila amesema kikosi chake kinampa matumaini ya kufanya vizuri na hata kumaliza msimu kwenye nafasi za juu na hali inayotokea hivi sasa ni upepo tu.

“Huu ni upepo mbaya naamini utapita Ihefu ni moja ya timu imara na shindani kupoteza mechi nne mfululizo inaumiza lakini bado tuna nafasi ya kurekebisha makosa yetu na kufanya vizuri ,” amesema Mwambusi.

Kocha wa Ihefu, Juma Mwambusi.

Amesema kwa sasa anachokifanya ni kuwajenga wachezaji kisaikolojia sababu hata wao wanayachukia matokeo mabaya wanayoyapata na wana pambana kutafuta ushindi lakini imekuwa ngumu.

Timu hiyo ya mkoani Mbeya inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi bila pointi katika michezo minne iliyocheza.

Ihefu imefungwa mabao 2-1 na KMC baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Mtibwa Sugar, imefungwa bao 1-0 na Namungo na kupoteza dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi.

Related Articles

Back to top button