Ligi Kuu

Mwaisabula aipa nafasi Yanga

DAR ES SALAAM: KOCHA na mdau wa soka Kennedy Mwaisabula amesema anaipa nafasi Yanga kushinda katika mchezo wa derby ya Kariakoo utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza na SpotiLeo Mwaisabula ambaye aliwahi kuitumikia Yanga miaka ya nyuma amesema Yanga imebebwa na wachezaji wengi wazoefu na wenye uwezo.

Amesema sio kwamba anaibeza Simba ila wote wako vizuri isipokuwa uzoefu wa wachezaji kwenye mechi hiyo unaweza kuipa nafasi ya kushinda Yanga.

“Ni mechi ambayo wachezaji wote wanajua ni ngumu na lazima wajitume. Yanga pamoja na mabadiliko ya makocha mara kwa mara bado ina wachezaji wanaoweza kuamua mechi,

“Lakini wanaweza kuamua mechi kama Simba watakuwa wazembe
kwenye safu ya ulinzi kwa kuwa mara nyingi wamekuwa na matatizo wakifanya makosa ya ajabu,”amesema.

Amesema faida iliyopo kwa Yanga wanatafuta sare au ushindi lakini Simba watakuwa kwenye presha ni lazima washinde ili kujiweka pazuri zaidi kwenye kinyang’anyiro cha kuwania taji la Ligi Kuu.

Mwaisabula amesema Simba wakipunguza makosa kati ya safu ya ulinzi na kipa lakini pia, uzembe wa wachezaji wao kutotumia nafasi wanazopata katika mechi kama hiyo basi wanaweza kushinda.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button