Muziki

Kiba, Mondi mbona safi tu

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo fleva nchini Ali Kiba ‘King Kiba’ amesema kuwa hakuna ugomvi baina yake na msanii mwenzake Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ wasichujua watu ni ushindani wa kazi zao ndio wanaona kama kunachuki baina yao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Crown Tv amesema kuwa hakuna ugomvi wala chuki baina yake na Diamond Platnumz watu ndio wanawagombanisha.

“Sijawai kusema wala kumwambia mtu kuwa nina ugomvi na msanii mwenzangu yoyote labda ushindani wetu wa biashara ndio sababu watu wanasema maneno yao wenyewe.

“Kazi zetu ndio zinazotupambanisha pamoja na mashabiki zetu binafsi sina ugomvi na msanii mwenzangu yoyote yule ni kazi tu ndio zinatushindanisha.

Pia ameongeza kuwa Msanii wa lebo ya Wasafi Mbosso Khan na Abdul Kiba ni marafiki kabla hata Mbosso kuwa kwenye lebo hivyo kufanya kazi nimebariki.

“Sitamzuia msanii wa King Music kufanyakazi na msanii yoyote kinachotakiwa ni kazi nzuri ambayo inaingiza pesa kwenye lebo na kuwapa mashabiki muziki mzuri.”amesema Alikiba

Related Articles

Back to top button