
MTOTO wa aliyekuwa mwanamuziki Remmy Ongala, Aziza Ongala amesema msimu wa tano
wa tamasha la Ongala utakuwa wa kipekee na mabadiliko makubwa.
Akizungumza na gazeti la HabariLEO, Aziza amesema tamasha hilo litakuwa la siku tatu
ambalo litashirikisha wanamuziki na wafanyabiashara katika muziki.
Amesema mwanzo walikuwa wakihakikisha wanafanya tamasha tofauti katika muziki, lakini
kwa sasa wamewekeza hadi katika biashara zingine za muziki.
“Lengo kubwa la tamasha ni kuuenzi muziki wa Dokta Remmy na maisha yake, lakini pia
kutengeneza jukwaa la kimataifa kwa ajili ya vijana wanaofanya muziki,” amesema.
Tamasha hilo linatarajia kuanza Novemba 24 na kukamilika Novemba 26 katika fukwe za Kawe, Dar es Salaam.