Habari Mpya

Haaland aanza safari ya magoli 1000

MANCHESTER: Mshambuliaji wa Manchester city Erling Haaland amefunga bao lake la 100 katika mchezo wa ligi kuu ya England dhidi ya Arsenal katika dimba la Etihad mjini Manchester.

Goli hilo la dakika ya 9 linamfanya Haaland kutimiza idadi ya mabao 100 akiwa na jezi ya Manchester City baada ya kucheza michezo 105.

Bao la kwanza kwa Haaland akiwa viunga vya Etihad lilikuwa la penalti dhidi ya West Ham united kabla ya kufunga kwa njia ya kawaida katika mchezo huo huo na kuiwezesha City kushinda bao 2-0

Haaland alisajiliwa na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya England akitokea Bundesliga katika klabu ya Borussia Dortmund mwanzoni mwa msimu wa 2022/23.

Related Articles

Back to top button