Upepo wa ubaya ubwela watua matawini, moto kuwaka Mwembeyanga Jumapili
DAR ES SALAAM : KATIKA Kuhakikisha wanaimarisha umoja na ushirikiano, viongozi wa Simba wameandaa bonanza la mechi za matawi kwa matawi, linalofanyika Jumapili hii uwanja Mwembe Yanga, Temeke, jijini.
Akizungumza na Spotileo, Meneja wa Idara ya habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema lengo la kuandaa Bonanza hilo ni kuimarisha Umoja wa matawi ya Simba.
“Bonanza hili kwa ajili ya kutengeneza mshikamano wa matawi kwa matawi , hakuna tawi bora kuliko mwengine maana wote wako katika mwamvuli mmoja wa Simba,” amesema Ahmed.
Bonanza hilo linafanyika kwa mara ya tatu kufanyika baada ya msimu uliopita kuchezwa kwenye fukwe ya Coco na Tawi la Simba Damu Fans (SDF) ya Tabata walikuwa mabingwa wa msimu huo .
Safari hii Mabingwa hao watetezi wanatarajia kucheza dhidi ya Simba Hatari na mechi ya Derby itakuwa kati ya Asilia ya Simba dhidi ya Nguvu ya Simba asilia mshindi wa mchezo huo atacheza na wasanii wanaoshabiki Simba.
Mechi zingine ni wakwanza sisi dhidi ya Ukonga Mazizini, Kijiwe Samli dhidi Karume Unstoppable, Wekundu wa Mtongani watacheza na Wekundu wa Terminal, Mpira Pesa Mikumi dhidi ya Kamati ya Robo Mbaya.
Tawi la Chui dhidi ya Wekundu wa Kijichi, Tunawakera watacheza na Simba Burudani kutoka Arusha , Shibam dhido ya Mpira Maendeleo na kutakuwa na mechi maalum ya Wanawake.