Habari Mpya

Muigizaji Mbunge azua jambo Ghana kuhusu tumbaku na bangi

GHANA: MUIGIZAJI na Mbunge wa Ayawaso West Wuogon, nchini Ghana John Dumelo amezua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuguswa na uharibifu wa hivi majuzi wa magunia 61 ya bangi uliofanywa na polisi.

Aprili 3, 2025, Jeshi la Polisi la Mkoa wa Volta liliteketeza magunia 61 yaliyokuwa na vifurushi 40 vya dawa hiyo haramu ili kuzuia dawa hizo zisiingie tena sokoni.

Hata hivyo, akijibu habari hizo, Dumelo aliandika katika ukurasa wake wa X na kwamba; “… lakini sigara ni halali nchini Ghana.”

Maoni yake yameibua mijadala kuhusu sheria za dawa za kulevya nchini Ghana, hususan Sheria ya Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya ya 2020, ambayo inaruhusu matumizi ya bangi ya kimatibabu na viwandani chini ya leseni kali lakini inapiga marufuku matumizi yad awa hizo kiburudani.

Wakati mamlaka ikizuia uhalifu, wakosoaji kama Dumelo wanasema kuwa sera hiyo haiendani, kutokana na hatari zinazojulikana za kiafya za tumbaku, ambayo bado inapatikana kisheria.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button