Habari Mpya

Ahmed:mambo safi lakini tunaenda Libya kwa tahadhari

MENEJA Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally ametoa tahadhari kwamba, licha ya kuwa wamejiandaa vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho lakini wanakutana na wapinzani wagumu.

Simba wanakwenda kukutana na Al Ahli Tripoli ya Libya mchezo utakaochezwa Jumapili ambapo licha ya Wekundu hao wa Msimbazi kuwa na matarajio makubwa lakini kazi haitakuwa rahisi sana.

Akiwazungumzia wapinzani wao, Ahmed Ally alisema :” Wana Simba tumjue vema mpinzani wetu tunaecheza nae mechi ya Kombe la Shirikisho. Ahly Tripoli ni klabu ya pili kwa mafanikio Nchini Libya lakin ndio klabu yenye mafanikio zaidi kimataifa nchini kwao.

Mafanikio yao makubwa ni kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika mwaka 2022 na Robo fainali ligi ya mabingwa Afrika 2017. Msimu uliopita walimaliza nafasi ya tatu, Kufuatia kutoridhishwa na matokeo hayo, wakafanya usajili mkubwa ili kurejesha heshima yao,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa miongoni mwa usajili wa kushtua waliofanya ni Mabolulu ambae amesajiliwa kwa dau la Bilioni 4 na inatajwa kuwa ndio usajili mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo.

“Kwa maelezo haya machache ni ishara kuwa tunaenda kukutana na mpinzani mgumu kweli kweli hivyo basi Wana Simba tuanze kujipanga vema kwa vita hii,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa mchezo wa kwanza ni Jumapili, Septemba 15 (Jumapili), Mechi hii ya ugenini wanawategemea zaidi wachezaji wao wapambane kadri ya uwezo wao na kutafuta matokeo ya ushindi.

“Mechi ya pili ni Septemba 22 Benjamin Mkapa hii inatutegemea sisi Mashabiki kuipeleka Simba yetu hatua ya makundi, katika Matawi yetu, Makundi yetu, Vijiwe vyetu mipango ya kuuvamia Uwanja wa Mkapa ianze sasa, tuanze kuhamasishana kwenda Uwanjani Sept 22. Maamuzi ya kwenda Makundi yapo mikononi mwetu wana Simba,” amesema Ahmed.

Related Articles

Back to top button