Sakata la Kagoma: Fountain Gate yawanawa Wananchi
DAR ES SALAAM: UONGOZI wa Fountain Gate umeweka wazi kuwa Yanga wamekiuka makubaliako yao kuhusu usajili wa kiungo Yusuph Kagoma ambaye kwa sasa usajili wake Simba ni mjadala mkubwa nchini.
Ofisa habari wa Fountain Gate FC, Issa Liponda ‘Mbuzi’, amekiri kulikuwepo na mazungumzo na makubaliano yalifanyika kati ya Rais wa timu hiyo Japhet Makau na Hersi Said wa Yanga kwa ajili ya manunuzi ya Kagoma.
Amesema makubaliano hayo yaliitaka Yanga ni kutoa Millioni 30 kipengelea namba 3.1 cha mkataba wa uhamisho uanaeleza malipo yatalipwa kwa awamu mbili kwa kuwapa miezi miwili Aprili na June kwa kipindi chote hawakulipa fedha hiyo.
“Fedha hizo zimelipwa Julai lakini haikuweka wazi wakati huo huo tulikuwa na makubaliano na Yanga kumnunua Kibabage kwa Million 30, Julai 6, tuliwataarifu Yanga kuvunja mkataba kwa kushindwa kulipa na kukubali kupokea malipo hayo kwa ajili ya kumnunua Kibabage ambaye Julai 4 walimtambulisha
Baada ya barua hiyo Yanga waliingiza Million 30 nyingine Julai 7 na tuliwaomba release ya Kagoma wakati tunafanya hayo, kuna dili la Simba limekuja na kumalizana nao na tukawapa realease letter huku Rais wa Yanga akahitaji fedha hizo walizingiza awamu ya pili wamchukue Azizi Andambwile.
Tumepokea kwa Yanga jumla ya Million 60, ambazo 30 kwa ajili ya Kibabage na zinzobakia za Andambwile, fedha za Kagoma hatujapokea na tunatambua ni mchezaji halali wa Simba,” amesema Ofisa habari huyo wa Fountain Gate.