EPL

Guardiola kumzuia Ederson kujiunga na Al-Nassr

MANCHESTER, Uingereza: MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola, anatazamia kumbakisha mlinda mlango, Ederson kabla ya msimu ujao na klabu hiyo itafanya jitihada za mwisho kumzuia kuondoka msimu huu wa joto licha ya kuwekewa fungu kubwa na klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia anayochezea nyoya Cristiano Ronaldo.

Al-Nassr wanadaiwa kumpa Ederson ofa ya pauni 900,000 kwa wiki pamoja na ada kubwa ya kusaini kuichezea klabu hiyo.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya  England wamepanga kumpa mkataba wa mwisho kipa huyo raia wa Brazil ili kumshawishi asielekee kwenye ligi hiyo inayomwaga pesa nyingi bila kujali umri wa wachezaji.

Kulingana na gazeti la The Sun, City wataweka ofa itakayokuwa na uamuzi kwa kipa huyo kuichukua ama kuiacha na hawatamzuia kama ataamua kuondoka Man City na kujiunga na Al-Nassr.

Ingawa City hawataweza kufikia ofa ya Al-Nassr, wanajipanga kutoa mkataba wa muda mrefu na nyongeza ya asilimia 75 ya mshahara wake uliopo.

 

Related Articles

Back to top button