EPL

Martinez ndo mpaka 2025/26

MANCHESTER:MASHETANI wekundu Manchester United wamethibitisha beki wao Lisandro Martinez atakosekana kwa muda wote uliosalia wa msimu huu wa 2024/25 kutokana na beki huyo kuumia kifundo cha mguu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Crystal Palace.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema baada ya uchunguzi wa kitabibu aliyofanyiwa beki huyo sasa wanatafuta njia iliyo bora zaidi ya kumtibu beki huyo muhimu ndani ya kikosi hicho.

“Tathmini ya kina  ya njia sahihi ya kumtibia na muda atakaotumia ili kumkinga na majereha zaidi inafanyika. Manchester united na watu wote tunamtakia heri Lisandro Martinez na tunamtakia uponaji wa haraka na tutakuwa naye muda wote atakaotuhitaji” imesema sehemu ya taarifa hiyo

Martinez mwenye miaka 27 alitolewa nje kwa machela dakika za lala salama katika mchezo ambao timu yake ilipotea 2-0 kwa Crystal Palace nyumbani Old Trafford.

Habari hizi ni pigo kwa kocha Ruben Amorim ambaye anajitahidi kurejesha makali ya kikosi hicho kilichopo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa imepoteza michezo saba kati ya 13 ya nyumbani msimu huu. Ikiongeza maswali na wasiwasi hasa baada ya beki mwingine wa klabu hiyo kukosa utimamu na hajapata kuanza hata mchezo mmoja wa ligi msimu huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button