Filamu

Filamu ya Spider-Man 4 kupata muongozaji mpya

HOLYWOOD: KUFUATIA mafanikio makubwa ya filamum ya Spider-Man: ‘No Way Home’, kilichokuwa kikizungumzwa ni nani atachukua jukumu la kuongoza filamu ya Spider-Man 4 na hadithi yake itakuwa na visa gani?

Sababu ya kutafutwa kwa muongozaji mpya ni kwa sababu ya muongozaji wa filamu za Spider Man Jon Watts kutotaka kuongoza filamu hiyo yenye muendelezo kwa ajili ya Spider-Man 4 huku akiwataka waongozaji wengine kujitokea kwa ajili ya kazi hiyo.

Muandaaji huyo mpya anatakiwa kutambua namna atakavyomchezesha Tom Holland anayecheza kama Spider-Man.

Utawala wa Tom Holland ulianza na mwonekano wa kwanza katika kampuni ya sinema ya Marvel Cinematic Universe mwaka 2016 akiwa katika filamu ya ‘Captain America’ na ‘Civil War’ kabla ya kuzindua filamu yake ya pekee mwaka uliofuata na ‘Spider-Man: Homecoming’.

Licha ya kuzindua filamu hiyo ndipo ukawa mwanzo wa muendelezo wa filamu nyingine zenye uhusika wa Spider man akitoa Spider-Man: ‘Far From Home’ ya 2019 na Spider-Man: ‘No Way Home’ ya 2021, na kila filamu ikawa na mafanikio makubwa zaidi yaliyosababisha ushindi mkubwa wa filamu zinazoongozwa na muongozaji huyo kutambuliwa kama filamu bora zaidi.

Ingawa hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanywa, Cretton yuko kwenye mazungumzo ya mapema na studio inayofanya kazi hiyo.

Makubaliano pia yanaendelea kwa sasa kwa Holland na Zendaya, ambao wamekuwa wakijadiliana na watayarishaji na watendaji wakati wa kutengeneza muendelezo huo.

Imeelezwa kwamba waandishi wawili Chris McKenna na Erik Sommers wanarejea kwa majukumu ya uandishi wa skrini huku Kevin Feige wa Marvel na Amy Pascal wa Sony watatoa filamu hiyo.

Related Articles

Back to top button