Filamu

Filamu 3,000 zapokelewa ZIFF 2024, 70 kushindanishwa

UONGOZI wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) limetangaza filamu 70 zilizopitishwa kugombea tuzo katika tamasha hilo linalotarajiwa kuanza Agosti 1 hadi 4 visiwani Zanzibar.

Kabla ya mchujo huo filamu zaidi ya 3,000 zilipokelewa katika tamasha hilo lililoanzishwa mwaka 1997 na zikachujwa hadi kupatikana filamu hizo zitakazoshindanishwa katika vipengele vya:
Filamu bora ndefu, filamu bora ya uhalisia, tuzo ya emerson kwa filamu bora ya zanzibar, filamu bora fupi, katuni bora, filamu bora ya aftika mashariki, mwigizaji bora wa afrika mashariki, meigizaji bora wa kike afrika, mwigizaji bora wa kiume na wakike tanzania, tuzo ya mwenyekiti wa ziff na tuzo ya mafanikio ya maisha pamoja na tuzonya chaguo la watu.

Kaulimbiu ya tamasha hilo ni Kuhuisha likiwa na lengo la kuongeza uelewa wa tasnia ya filamu na kukuza sanaa hiyo barani Afrika na kwa Nchi za majahazi.

Mchanganuo wa filamu hozo zilivyopokelewa kabla ya mchujo ni filamu 354 zimepokelewa kutoka nchi za Afrika. Ambapo Kenya imewasilisha filamu 169, Uganda filamu 123, wakati Tanzania filamu 62, Rwanda 12 Burundi 3 na Afrika Kusini 71 huku filamu zilizochaguliwa ni pamoja na filamu ndefu 17, zinazoonesha hali halisi 13, filamu fupi na katuni 30.

Uongozi wa ZIFF pia umeonyesha masikitiko yake kushindwa kufanya Mashindano ya Tuzo za Filamu za Maendeleo ya Sembene Ousmane kwa mwaka huu kutokana na mdhamini kujiondoa katika hatua za mwisho.

Ziff pia imezindua Bango la Tamasha la 27 huku ikiandaa program maalum kwa watengeneza filamu ambapo watafundishwa kutengeneza filamu kwa kutumia simu.

Related Articles

Back to top button