Filamu

Devotha Mayunga aiomba serikali kuiangalia sekta utayarishaji filamu

MTAYARISHAJI wa Tamthilia ya Toboa Tobo, Devotha Mayunga ameiomba serikali kuifanya sekta ya utayarishaji wa filamu kuwa rasmi ili kuleta unafuu kwenye baadhi ya mambo.

Akizungumza na HabariLEO, Devotha ambaye pia ni muongozaji wa filamu amesema kama serikali itafanya sekta hiyo kuwa rasmi na kutambulika kama ajira huenda ikapunguza mlolongo katika kupata ruhusu kwenye baadhi ya maeneo.

“Tutambulike kama ajira rasmi, ili itusaidie kupata ruhusu kwenye baadhi ya maeneo na ipunguze mlolongo kuwa mrefu kwenye baadhi ya vitu,” amesema Devotha Mayunga.

Devotha Mayunga kwa sasa ni mtayarishaji na muongozaji wa tamthilia ya Toboa Tobo.

Related Articles

Back to top button