Filamu

Msimu Mpya wa ‘Kash Money’ ya Kenya kwenye Netflix

KENYA: KUONGEZEKA kwa ubora wa filamu na tamthilia za Kenya kumeshawishi mtandao wa Netflix kuionesha kwa mara ya kwanza tamthilia ya ‘Kash Money’ katika msimu mpya Januari hii.

Onesho hilo linalohusu mada ya nasaba yenye nguvu ya familia, linajumuisha wasanii mashuhuri, wakiwemo waigizaji mashuhuri wa Kenya wakiwemo, John Sibi-Okumu, Sanaipei Tande, Amara Tari, Lenana Kariba, Makbul Mohamed, Janet Mbugua, Morris Mwangi, Dedan Juma, Joey Muthengi na Oliver Litondo.
Tamthilia hiyo imeandaliwa, imetayarishwa na kuongozwa na Phil Bresson na Grace Kahaki wa Insignia Productions.

Tamthilia hiyo inaeleza mfululizo wa kuvutia wenye matukio ya siri, changamano, usaliti na matukio ya kishirikina ndani ya familia. Pia inaelezea mada changamano kama vile uchoyo, siri na tamaa, ikielezea changamoto kubwa ya kusaka pesa.

Wadau mbalimbali walioshuhudia ‘trela’ la tamthilia hiyo wamekuwa na matumaini ya kufanya vizuri katika sekta ya tamthilia duniani.

Related Articles

Back to top button