BurudaniFilamu

Lulu achekelea kuyamaliza na Mama Kanumba

DAR ES SALAAM: Msanii wa Filamu Elizabeth Michael, ‘Lulu’ amesema kuwa anafuraha na amani kupatana na Mama wa Marehemu Steven Kanumba.
Lulu amesema ni muda mrefu tangu wapitie changamoto lakini kwa sasa anafurahi wapo sawa.
“Namshukuru Mungu kwa tulipofikia ninafuraha na mama anafurahi pia ni kitu cha kumshukuru Mungu kwa yote tuliopitia na hapa tulipo fika vingine vyote vya kibinadamu ni mzazi ana haki ya kujisikia vyovyote anavyojisikia simlaumu.”
“Kuongea chochote kwa wakati wowote anapohitaji kujisikia vizuri.”
 
“Mara nyingi nasemaga huu ni msalaba wangu nitaubeba na utakuwa chini ya mabega yangu siku nitakapokuwa sipo duniani nitadili nao kwa namna utakapo kuja.”
“Mama yangu anafuraha sasa hivi simlaumu kwa Lolote wala nini ni hali inayomkuta kwa muda fulani japo sisi hatujisikii kama yeye.” amesema Lulu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button