Diamond League kuwajaza ‘Minoti’ wanariadha 2025
*Diamond League kuwajaza fedha nyingi wanariadha 202*
Na Festo Polea
WANARIADHA wataweka mfukoni pesa zaidi katika msimu wa Ligi ya Diamond wa 2025 baada ya kutangazwa kwamba pesa za zawadi watakazopewa zitaongezwa.
Wanariadha wamekuwa wakipata dola za kimarekani 30,000 kwa kushinda katika fainali na dola 10,000, lakini kiasi hicho kwa mwaka 2025 kitaongezwa kwa kiasi kikubwa.
Hii inakuja wakati mijadala kuhusu pesa za zawadi na ushindani kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo huku kampuni nyingine zikiahidi kuongeza fedha kwa wakimbiaji watakoshiriki katika mashindano yao.
Wanda Diamond Ligi wametangaza kuwa mnamo 2025, msimu wa 16, pesa za mikutano zitakuwa dola za kimarekani 500,000 na dola 2,240.
Kwa hivyo, pesa za zawadi kwa kuonyesha nidhamu katika mikutano zitakuwa kati ya dola 30,000 na dola 50,000 na huku katika fainali zikiwekwa kati ya dola 60,000 na dola100,000.
Wanariadha sita wa Kenya walishashinda dola 30,000 katika fainali ya Ligi ya Diamond iliyokamilika hivi karibuni mwaka 2024. Fadha hizo zinaelezwa kwamba huenda zimewekwa kwa lengo la kuvutia nyota wenye majina makubwa katika riadha kushiriki.