Kwingineko

Cristiano Ronaldo kuwa kocha ama la?

SAUDI ARABIA: BAADA ya kufungua channel yake ya Youtube ambayo kwa sasa ina zaidi ya wafuatiliaji milioni 48.5 na watazamaji zaidi ya milioni 282.4,wadau wengi wamekuwa na maoni tofauti juu ya kazi atakayofanya mkali huyo wa soka baada ya kustaafu kucheza soka.

Cristiano Ronaldo kwa sasa anakipiga na Al-nassr ya Saudi Arabia lakini baada ya kustaafu soka anahusishwa na kuwa kocha wa kiwango cha juu katika ufundishaji baada ya kuonekana wakati wa ushindi wa Ureno wa Euro 2016, ambapo alionekana akiwaongoza wachezaji wenzake kwa bidii pamoja na kocha wa wakati huo Fernando Santos, lakini nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United bado hajashawishika kuwa kocha.

Akiwa na umri wa miaka 39, Ronaldo anayeshikilia tuzo 5 za Ballon d’Or, ameonyesha mashaka yake ya kuwa kocha pindi atakapomaliza soka lake kama mchezaji.
“Ni vigumu sana… usiseme kamwe,” Ronaldo alisema katika mahojiano na tovuti rasmi ya FIFA (kupitia beIN Sports).

“Sijui nini kitatokea katika siku zijazo, lakini kwa wakati huu, sijioni kuwa kocha.”
Alisema Ronaldo msimamo wake ukionyesha kusitasita kufuata njia iliyochukuliwa na magwiji wengi wa soka ambao walibadilika na kuwa makocha.
TUKO.co.ke iliripoti kuwa Ronaldo alifunga bao lake la 50 kwenye Ligi ya Saudia wakati wa mechi ya ufunguzi ya Al-Nassr msimu wa 2024/25.

Msimu uliopita Ronaldo aliweka rekodi mpya, akifunga mabao 35 katika mechi 31 ,idadi ya juu zaidi katika msimu mmoja.

Related Articles

Back to top button