‘Stress’ za Son Tottenham zinaishia nyumbani

GOYANG, SOUTH KOREA, Nahodha wa Tottenham Hotspur Son Heung-Min amesema kurejea nyumbani kwao South Korea kwenye michuano ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia la 2026 kunampa furaha na nguvu kubwa baada ya mwenendo usioridhisha wa Tottenham kwenye Ligi Kuu ya England.
Son ambaye yuko nchini humo kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Oman na Jordan anatarajia kulisaidia taifa hilo kufuzu moja kwa moja iwapo ataliongoza kushinda michezo yote miwili.
“Hata kama nimekuwa na wakati mgumu sana Tottenham Hotspur, kuja nyumbani na kuona mashabiki wetu napata furaha na nguvu mpya. Ninafurahi kuwa leo mashabiki zaidi watakuja na kutushangilia na sisi hatutawaangusha. Huu ni mchezo wetu wa kwanza mwaka huu na tutafanya liwezekanalo tushinde.” Son ameviambia vyombo vya habari nchini Korea
South Korea itacheza Michezo miwili, dhidi ya Oman mchezo utakaopigwa baadae leo mjini Goyang na dhidi ya Jordan siku tano baadaye mjini Suwon nchini humo ambapo iwapo watashinda watajihakikishia nafasi kwenye kombe la dunia lijalo nchini Marekani, Mexico na Canada.
Katika EPL timu yake ya Tottenham Hotspur haina mwenendo mzuri ikiwa nyuma ya Chelsea wanaoifunga top 4 kwa pointi 15 huku wakitarajia kukutana April 5 na wakiwa wameondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA huku matumaini ya kutwaa taji msimu huu ikiwa ni Europa League