Chelsea yakerwa na vipigo

LONDON, Meneja wa Chelsea Enzo Maresca amesema yeye, wachezaji na viongozi wanakerwa na mfululizo wa matokeo mabaya ambayo timu hiyo imekuwa ikipata na kwamba wanahitaji kuamka kama wanataka kufufua matumaini yao ya kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu ya England yenye ushindani mkubwa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Aston Villa Jumapili, mchezo utakaopigwa ugenini katika dimba la Villa Park mjini Birmingham nchini England amesema
“Tunachukizwa sana, kwakweli hatuyapendi matokeo tunayopata. Sote tunafahamu kuwa tupo kwenye klabu inayoshindania makombe sio kubaki ligi kuu. Tupo kwenye kipindi kigumu, wachezaji hawa ndio walikuwa nafasi ya 4 katika mechi 19, 20 naamini baada ya kipindi hiki watarejea kwenye ubora wao” amesema kocha huyo.
Chelsea wapo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi pointi moja nyuma ya Manchester City walio nafasi ya 4 na Bournemouth aliye katika nafasi ya 5 baada ya vijana hao wa Maresca kushinda michezo miwili kati ya tisa waliocheza hivi karibuni.
Chelsea walibondwa 3-0 na Brighton kwenye mchezo wa weekend iliyopita na hawajashinda mchezo wowote wa ugenini kwenye Premier League tangu walipowafunga Tottenham 4-3 Desemba 8 mwaka jana.