EPL

Tabu iko pale pale

MENEJA wa mabingwa mara 4 mfululizo wa Ligi kuu ya England Manchester city Pep Guardiola, anatarajia kuongeza mkataba wa kusalia Etihad hadi mwishoni mwa msimu wa 2025/2026 baada ya kukubali kuongeza mkataba na wababe hao wa jiji la Manchester.

Meneja huyo wa zamani wa FC Barcelona na Bayern Munich alitarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu lakini kumekuwa na tetesi za mtaalamu huyo wa soka kuongeza mkataba kabla ya jarida la The Athletic kuripoti mapema leo kuwa Pep amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Manchester City wamekuwa na mwenendo mbovu siku za hivi karibuni baada ya kupoteza michezo minne mfululizo ikiwa ni rekodi iliyotia doa CV nzuri ya kocha huyo kwani hapo awali hakuwahi kupoteza mechi nne mfululizo katika maisha yake ya ukocha.

Chini yake Manchester City imetwaa ubingwa mara 6 wa ligi kuu ya England huku akiifanya klabu hiyo kuwa klabu ya kwanza na ya pekee kutwaa ubingwa wa ligi hiyo pendwa Duniani mara nne mfululizo.

Guardiola aliyewasili Etihad mwaka 2016 ameshinda mataji 15 katika misimu 8 Manchester City mataji yanayojumuisha ubingwa wa Ligi Kuu mara 6, mawili ya kombe la FA, makombe manne ya Carabao, moja klabu bingwa barani Ulaya, moja klabu bingwa ya dunia na UEFA super cup moja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button