EPL

Arsenal yamwachia Emile Smith Rowe

ENGLAND: Klabu ya Arsenal imemuuza aliyekuwa mchezaji wao Emile smith Rowe kwenda klabu ya Fulham.

Fulham imetoa kitita cha pauni milioni 34, ada ambayo imeweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyesajiliwa kwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo.

Klabu hiyo imetoa pauni milioni 27 na nyingine milioni 7 kama ‘ad-ons’ kwa mchezaji huyo ambaye anaweza kuichezea klabu hiyo mchezo wake wa kwanza siku ya jumatatu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla.

Smith Rowe aliondoka katika kambi ya Arsenal mapema wiki hii na kwenda kukamilisha vipimo kisha akajiunga na kikosi cha Fulham kilichopo nchini Ureno.

Smith Rowe, 24,ameichezea Arsenal michezo 25 tu toka mwezi agosti 2022 baada ya kutokuwa na nafasi katika kikosi hicho kinachonolewa na Mikel Arteta.

Washika mtutu hao wa London wanamuachia kiungo huyo wakiwa wametoka kukamilisha usajili wa beki Riccardo Calafiori na sasa wanamfukuzia kiungo wa Real Sociedad na Hispania, Mikel Merino.

Uuzaji wa Smith Rowe ni wa pesa nyingi zaidi kwa Arsenal toka walipomuuza Alex Oxlade- Chamberlain kwenda Liverpool mwaka 2017.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button