BMT yawashika koo makocha na wachezaji wa kigeni

DAR ES SALAAM: BARAZA la Michezo la Taifa (BMT), lipo katika mchakato wa kuangalia jinsi ya kuongeza ada kwa wachezaji na makocha wa kigeni kulingana na kiwango kitakachowekwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Msajili wa vyama vya michezo kutoka BMT, Evordy Kyando amesema endapo TFF na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) wakiongeza ada kwa makocha na wachezaji, watalazimika kubadilisha mfumo kutoka kulipa kiasi cha fedha na kuweka asilimia ya kile wanacholipa.
“Klabu au shirikisho linalipa dola elfu 5 kwa makocha na wachezaji wapya ambao ni mara ya kwanza kuja nchini, dola elfu 1000 kwa wanaotoka timu moja kwenda nyingine. Msimu ujao tunaangalia kuja kivingine tutachukuwa kwa dola lakini kwa asilimia ya kiasi cha fedha ambazo makocha hao na wachezaji wanatakiwa kulipa,” amesema.