Ligi Kuu

Mpanzu yupo sana Msimbazi

..aongezewa miaka miwili

DAR ES SALAAM: KLABU ya Simba imeondoa sintofahamu kuhusu hatma ya kiungo mshambuliaji wake, Elie Mpanzu, baada ya kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Mpanzu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), amekamilisha usajili huo leo Jumatatu, Machi 23, 2026, hatua inayomuweka Msimbazi hadi Desemba 2028.

Awali, kiungo huyo alikuwa kwenye mkataba wa miaka miwili ulioanza Januari 2025 na uliotarajiwa kumalizika Desemba 2026, hali iliyozua uvumi wa kuhusishwa na kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, uongozi wa Simba chini ya mwekezaji wake, Mohamed Dewji, umefunga mjadala huo kwa kumbakisha nyota huyo ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Hatua ya kumuongezea mkataba Mpanzu imeelezwa kuwa sehemu ya mkakati wa Simba kuendelea kuimarisha kikosi chake na kuhakikisha inakuwa na utulivu wa kutosha katika harakati zake za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu.

Related Articles

Back to top button