Ligi Kuu

Ubaya Ubwela kufanya yake Chuga?

ARUSHA: KLABU ya Simba SC itakuwa wageni wa wagosi wa kaya Coastal Union katika mchezo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara katika dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha katika mchezo ambao wekundu wa Msimbazi watakuwa kwenye vita ya kusaka pointi tatu ili kupunguza pengo la pointi baina yao na watani wao Yanga walio katika usukani wa Ligi.

Simba wanaingia katika mchezo huu wakiwa na kumbukumbu mbaya katika mzunguko wa kwanza baada ya Coastal Union kutoka nyuma dakika za jioni na kuvuruga uongozi wa 2-0 ambao simba waliushikilia tangu kipindi cha kwanza na vijana hao wa kocha Lazaro (wakati huo) kuondoka na pointi moja KMC complex Oktoba 4 mwaka jana.

Coastal Union hawana ubabe kabisa mbele ya Simba kwani katika michezo 11 iliyowakutanisha wamewapa Simba takriban pointi 27 na wao kuambulia tatu pekee. Mchezo baina ya Simba na Coastal Union haujawahi kuwa rahisi licha ya maneno juu ya uhusiano wao.

Simba wataingia kusaka ushindi ili kuongeza morali kuelekea mchezo wa dabi ya Kariakoo Machi 8 katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam. Swali linabaki je! Ubaya Ubwela kufanya yake Chuga?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button