Ligi KuuNyumbani

Ni mtanange wa watengeneza sukari vs mvinyo

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja kufanyika mkoani Morogoro.

Walima zababi kutoka makao makuu ya nchi, klabu ya Dodoma Jiji ni wageni wa walima miwa, Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani.

Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 26 baada ya michezo 22 wakati Dodoma Jiji ni ya 11 ikiwa na pointi 24.

Katika mchezo wa kwanza kati ya timu hizo uliofanyika uwanja wa Liti, Singida Oktoba 25, 2022 Mtibwa Sugar iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji.

Related Articles

Back to top button