
MATAJIRI wa Chamazi, Azam imefikia makubaliano na timu ya Raja Club Athletic kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Gambia mwenye umri chini ya miaka 23, Gibril Sillah.
Taarifa ya Azam imesema Sillah anatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa kumalizia taratibu za mwisho za usajili.
“Tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumefikia makubaliano na klabu ya @rcaofficiel, ya kumnunua kiungo wao mshambuliaji, @gsillah70,”imesema Azam.
Kwa mujibu wa Azam msimu uliopita wa Ligi Kuu Morocco Sillah amefunga mabao saba na kutoa pasi nne wakati akiwa kwa mkopo klabu ya JS Soualem ya Morocco.