Ligi KuuNyumbani

Yanga yashtukia mabadiliko Azam

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema hatua ya wapinzani wao katika mchezo unaofuta wa Ligi Kuu bara Azam kubadilisha benchi la ufundi kumeiongezea timu yake umakini katika maandalizi kuelekea mchezo huo Septemba 6.

Akizungumza na Spotileo, kocha huyo amesema wamestushwa na hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Azam ya kubadili kocha huku zikiwa zimebaki siku chache kabla ya timu hizo kukutana.

“Hofu yetu pengine kuna kitu wamekiona kuelekea mchezo huo ndio maana tumeongeza umakini na kuzidisha muda wa mazoezi na mbinu ili tuwe bora mara mbili zaidi ya tulivyopanga,” amesema Kaze.

Kwa mujibu wa Kaze mchezo huo utakuwa mgumu na wenye ushindani lakini maandalizi wanayoyafanya yanawapa matumaini ya kufanya vizuri kama ilivyokuwa mechi zilizopita.

Msimu uliopita Yanga iliifunga Azam mechi zote mbili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Related Articles

Back to top button