Habari Mpya

Azam FC yaipeleka Azamka Rwanda

DAR ES SALAAM: Matajiri wa jiji la Dar Es Salaam Azam FC wameamua kulipeleka tamasha lao la Azamka jijini Kigali nchini Rwanda wakiambatanisha tamasha hilo na tamasha la klabu la Rayon Sports ya nchini Rwanda tamasha ambalo litafanyika august 3 mwaka huu

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram klabu hiyo, Azam FC imetoa taarifa inayosema kuwa mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, itakayopigwa jijini Kigali, Agosti 3, mwaka huu kwenye Rayon Day, itaenda sambamba na siku yao ya Azamka ambayo kwa kawaida hutumika kutambulisha kikosi cha msimu mpya.

Klabu hiyo imeenda mbali na kuserma kuwa kupeleka siku hiyo jijini Kigali ni mkakati maalumu wa klabu hiyo kukuza brand yake ndani na nje ya Tanzania, wakisema kuwa jiji Kigali ni kituo tu cha kuanzia, huko mbeleni wataendelea kulifanya tamasha hilo katika nchi zingine.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button