Habari Mpya

Minziro ana matumaini kimataifa

Kocha wa Geita Gold, Fred Minziro.

KOCHA wa Geita Gold, Fred Minziro amesema matumaini ya kikosi chake kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa nimakubwa.

Akizungumza na Spotileo amesema maandalizi ya ya timu hiyo kuelekea mchezo wa kwanza dhidi ya Hilal Alsahil ya Sudan yanaendelea vizuri na wapo tayari kwa mchezo huo.

“Ni kweli hatujaanza vizuri msimu mpya wa Ligi Kuu lakini hicho siyo kigezo cha kuendelea kufanya vibaya kwenye ligi tunajua uzito wa mashindano ya Kombe la Shirikisho na tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Minziro.

Kocha huyo amesema kutoanza vyema kwa timu yake kwenye Ligi Kuu kumetokana na kuchelewa kuanza maandalizi lakini pia wachezaji wake kutokuwa na muunganiko mzuri.

Minziro amesema hana presha na hilo sababu ligi bado mbichi na Geita Gold ina nafasi kubwa ya kurekebisha makosa na kukaa inapostaili.

Geita Gold itaanza kampeni Kombe la Shirikisho Afrika ugenini dhidi ya Hilal Alsahil Septemba 11, Sudan na mchezo wa marudiano kupigwa Tanzania Septemba 17.

Related Articles

Back to top button