Habari Mpya

Mandojo Afariki dunia

Auawa akidhaniwa ni mwizi

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Joseph Francis maarufu Mandojo amefariki dunia.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba kifo chake kimetokea alipokuwa akikimbizwa hospitalini kutokana na kushambuliwa na watu wakimdhania kuwa mwizi.

Mmoja wa msanii waliokuwa wakiimba Pamoja kama kundi Domo Kaya amesema msanii huyo alifariki akiwa anakimbizwa hospitali na taarifa zaidi kuhusu msiba wake zitatolewa baadaye.

Domo Kaya amesema msanii huyo amefariki akiwa anatarajia kusherehekea miaka yake kadhaa siku ya Agosti 22 mwaka huu.

“King! Kasmodo MAN-DOJO daaaah! Mwanangu Mwanangu kabisa aisee hata siamini, 22nd mwezi huu ilipaswa kuwa siku yako ya kuzaliwa, Aisee kwa nini! !! Huzuni sana.”Mandojo na Domokaya walitoa nyimbo nyingi chini ya studio ya Bongo Record iliyokuwa chini ya P Funk Majani. Nyimbo hizo pendwa ni pamoja na Wanoknok, Nikupe Nini, Dingi, Taswira, Niaje, Nizikwe Hai na nyingine nyingi.

R.I.P Man Dojo.

Related Articles

Back to top button