La Liga

Arbeloa amjia juu mwamuzi

MADRID, Hispania KOCHA wa Real Madrid, Álvaro Arbeloa, ameonesha kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya FC Bayern Munich kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Arbeloa amesema beki wa Bayern, Jonathan Tah, alipaswa kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya rafu aliyomfanyia Kylian Mbappé.

“Sielewi kwa nini mchezaji wa Bayern hakutolewa kwa foul aliyomfanyia Mbappé. Haya ni maamuzi ambayo ni magumu kuelewa.”

Kocha huyo alikuwa akirejea tukio ambalo Tah alipitisha soli yake kwenye kifundo cha mguu wa Mbappé kwenye challenge ambayo haikuonekana kuwa ya makusudi, na mwamuzi aliamua kutoa kadi ya njano pekee.

Wakati huo huo, Madrid wamepata pigo jingine baada ya Aurélien Tchouaméni kuoneshwa kadi ya njano ambayo itamfanya kuukosa mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Munich.

Licha ya kupoteza mchezo wa kwanza, Arbeloa ameweka wazi kuwa bado ana imani kubwa na kikosi chake kugeuza matokeo hayo.

“Kama kuna timu moja inayoweza kushinda Munich, hiyo ni Real Madrid. Sisi ni Real Madrid.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button