Hansi Flick kocha mpya Barcelona

MIAMBA ya mpira w miguu Hispania, Barcelona imemteua kocha wa zamani wa Bayern Munich, Hansi Flick kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Flick, aliyetimuliwa ukocha timu ya taifa ya Ujerumani Septemba 2023, anachukua mikoba ya Xavi Hernández aliyeachishwa kibarua wiki iliyopita.
Katika taarifa Barcelona imesema imemchagua mtu anayefahamika kwa kuzifanya timu zicheze mtindo wa kushambulia kwa nguvu na kumiliki uliompa mafanikio makubwa ngazi ya klabu na kimataifa akishinda mechi mbalimbali.
“Mpendwa Hansi Flick, karibu kwenye klabu. Ni rasmi! 📝
Flick hadi 2️⃣0️⃣2️⃣6️⃣,” imesema Barcelona kupitia mitandao yake rasmi ya kijamii.
Kutimuliwa kwa Flick timu ya taifa ya Ujerumani kulikuja baada ya kuiongoza Bayern Munich kutwaa mataji matatu 2020, akinyakua taji la Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya mabingwa.
Kocha wa Barcelona anayeondoka Xavi, aliyeachishwa kazi mwezi mmoja baada ya klabu kuthibitisha atabaki, amesema mrithi wake “atateseka” katika jukumu hilo.
Barcelona imeshika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania-LaLiga msimu wa 2023/24 iliyofikia Mei 26 ikiwa na pointi 85 nyuma ya Real Madrid.