La Liga

Baena atua Atletico kwa Bilioni 156

MADRID: Taarifa kutoka nchini Hispania zinasema kuwa wababe wa soka nchini humo, Atletico Madrid wametumia kiasi cha Euro milioni 50 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 156.16 kumsajili kiungo wa kati wa Villarreal Alex Baena mwenye miaka 23 kwa mkataba wa miaka mitano.

Baena aliingia kwenye timu ya wakubwa ya Villarreal akitokea kwenye akademi ya vijana, akicheza kwa mara ya kwanza mwaka wa 2020 kisha kutumikia msimu mmoja kwa mkopo katika klabu ya Girona aliyoisaidia kupanda daraja na amekuwa na namba ya kudumu kikosini hapo.

“Nimefurahi sana, ni hatua kubwa katika maisha yangu ya soka. Ninajiunga na moja ya klabu kubwa nchini Uhispania na Ulaya,” Baena alisema.

Mchezaji huyo ameichezea timu ya taifa ya Hispania katika viwango vyote vya timu za vijana huku akicheza kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya wakubwa mwaka 2023, akifunga bao kwenye mechi yake ya kwanza huku akiwa sehemu ya kikosi kilichotwaa kombe la Euro 2024.

Baena, ambaye anacheza kama winga wa kushoto, pia alikuwa sehemu ya timu ya Spain iliyoshinda medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka jana, ambapo alifunga katika fainali dhidi ya Ufaransa. Akitajwa pia kwenye Kikosi Bora cha Msimu cha LaLiga 2024/25.

Related Articles

Back to top button