Lewandowski asherehekea kuzaliwa kwa staili

MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski na wachezaji wenzake wapya wa Barcelona wameonesha jinsi gani wanaweza kuwa hatari msimu huu baada ya timu hiyo kuichapa Real Sociedad mabao 4-1 huku Lewandowski akifunga mawili.
Siku hiyo pia ni kumbukumbu ya tarehe ya kuzaliwa ya Lewandowski.
Huo ni mchezo wa pili kwa Barcelona katika Ligi Kuu ya Hispania baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa kwanza dhidi ya Rayo Vallecano.
Lewandowski aliyesaini Barcelona msimu huu wa joto akitokea Bayern Munich amefunga mabao hayo dakika 1 na 68.
“Siku zote bao la kwanza ninalofunga katika timu mpya huwa kwa ajili ya baba yangu,” amesema Lewandowski baada ya mchezo huo.
Mabao mengine ya Bacelona yamefungwa na Ousmane Dembele dakika ya 66 na Ansu Fati dakika 79.
Bao pekee ya Sociedad limefungwa na Alexander Isak katika katika 6.