Mwanariadha afichua kitakachoifanya Kenya kushinda Dhahabu Jumuiya ya madola

NAIROBI : Mwanariadha wa Kenya anayeshiriki mbio za kuruka viunzi na maji mita 3,000, Simon Koech, amesema ushindi alioupata kwenye mbio za Diamond League jijini Monaco umempa imani kubwa ya kuwania medali ya dhahabu katika Michezo ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth Games) itakayofanyika Glasgow, Scotland mwaka huu.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 22 amesema matokeo hayo yamemthibitishia kuwa yuko katika kiwango bora kuelekea mashindano hayo makubwa na kuiwezesha Kenya kubeba medani ya dhahabu.
Koech alishinda mbio hizo kwa muda wa dakika 8:03.35, akiwapiku Mjapani Ryuji Miura na Mkenya mwenzake Edmund Serem. Baada ya ushindi huo, alisema licha ya hali ya hewa ya joto nchini Monaco, alijituma kuhakikisha anamaliza mbio akiwa mshindi, huku akisisitiza kuwa ushindi huo umeonesha mwili wake uko tayari kwa changamoto inayofuata.
Mwanariadha huyo amesema lengo lake kubwa sasa ni kuipa Kenya medali ya dhahabu katika Commonwealth Games, akieleza kuwa anafahamu maeneo ambayo bado anapaswa kuyaboresha kabla ya mashindano hayo. Ataiongoza timu ya Kenya katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji pamoja na Edmund Serem na Leonard Bett, huku akiamini kizazi kipya cha wanariadha wa Kenya kina uwezo wa kuendeleza ubabe wa taifa hilo katika mchezo huo.
Koech amekuwa na msimu mzuri mwaka 2026 baada ya kushika nafasi ya pili kwenye Kip Keino Classic, kumaliza wa tatu katika Diamond League ya Rabat, na baadaye kujihakikishia nafasi ya kuiwakilisha Kenya kwa kushinda mchujo wa taifa. Sasa macho yake yote yameelekezwa Glasgow, ambako anatarajia kutimiza ndoto yake ya kutwaa medali ya dhahabu na kuendeleza heshima ya Kenya katika mbio za kuruka viunzi na maj




